Mwanzo 1:20

Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.

Mwanzo 1:12

Nchi ikaota majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake,na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

Zaburi 24:1-2

Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake. Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mti ya maji aliithibitisha.

Yoeli 2:1

Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi na watetemeke; Kwa maana siku ya Bwana inakuja. Kwa sababu inakaribia.

Yeremia 1:18-19

Maana, tazama, nimekufanya leo kuwa mji wenye boma, na nguzo za chuma, na kuta za shaba; juu ya nchi yote; juu ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wa nchi hii. Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema BWANA, ili nikuokoe.

Thursday, February 13, 2014

KIBALI

Watashindana! Lakini hawatashinda.

Uhali gani mpenzi msomaji wa mtandao huu unaokujuza mengi yaendeleayo madhabahuni mwa Bwana GRC Ubungo Kibangu.

Kama kawaida katika kila siku ya Alhamisi kama ya leo, huwa kuna ibada ya maombezi ambayo hungozwa na mtumishi wa Mungu, Mchungaji Antony Lusekelo, ambapo katika siku ya leo, somo kuu lilikuwa ni juu ya kibali.

Hizi ndo sifa za kibali, kibali utengenezwa na nini, na baadhi ya watu waliyokuwa na kibali katika Biblia

Sifa za kibali;

Humpa mtu kusikilizwa, kuaminika, kupendwa, kuthaminika n.k

Kibali hutengenezwa na nini?

Kibali hutengenezwa na tabia ya mtu binafsi, mfano kwa kuwa na roho nzuri, tabia nzuri, kujituma, kujali, msafi, n.k.

Baadhi ya watu waliyokuwa na kibali katika Biblia.

Daniel - Na ndiyo maana kibali hicho kilisababisha Nebukardeza mfalme wa nchi, kumsujudia.
(Soma Daniel 3)

Yusufu-  Ndiyo maana alipelekwa kwa Potifa kama mtumwa ili ajifunze uongozi.

Musa- Ndiyo maana akapata nafasi ya kuingia katika ikulu ya Farao na akapata elimu ya kutosha uongozi.

Baada ya somo hilo zuri maombezi ya nguvu yaliendelea na tulimsifu sana Mungu kwa pamoja na Mzee wa Upako.

Thursday, January 2, 2014

`Ninaupika mwaka 2014 kwaajili yako` asema Mzee wa upako.


Shalooom!

Ninakusalimu kwa Jina la Bwana Yesu Kristo aliyetufia msalabani. Karibu tuweze kujuzana yale yaliyojiri madhabauni mwa Bwana katika siku hii ya leo, ikiwa ni alhamisi ya kwanza kabisa ya mwaka 2014.

Leo kama kawaida ibada ilianza kwa sifa na kuabudu na baada ya muda, Mzee wa Upako alipanda madhabahuni na kuanza kuhudumu.

Baada ya kuongoza nyimbo za kuabudu na kusifu kama ilivyo kawaida yake, Mzee wa upako aliendeleza utabiri wake wa mwaka jana mwishoni, yaani wiki iliyopita, wa kuwa maisha ya kila mmoja atayaombea ili yaweze kubadilika, na kusema kuwa ataupika mwaka huu ili mambo yawe DOUBLE DOUBLE, kisha akausindikiza utabiri huo kwa mahubiri ya jinsi Mungu alivyo mtumia Musa katika kuwaokoa wana wa Israeli.

Aidha mtumishi wa Mungu, Mch. Antony Lusekelo, alitoa mfano wa Samson pia wa jinsi alivyorudiwa na nguvu zake baada ya nywele zake kuanza kuota tena, na kusema kuwa kama ilivyokuwa kwake Samson ndivyo Mungu atakavyorudisha upya nguvu zetu za kiuchumi, mipango, afya na kadhalika ndani ya mwaka huu wa 2014.

Na baada ya mahubiri hao yaliyochukua saa mbili, mtumishi wa Mungu aliwaongoza watu katika ibada ya matoleo, na kisha kuwaombea mmoja mmoja  mpaka mwisho wa ibada.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa leo ibadani, japo kwa kifupi. Karibu sana Jumapili ili ujifuze mengi yatakayo kujenga kiakili, kiroho na hata kimwili.

Barikiwa sana!