Shalooom!
Ninakusalimu kwa Jina la Bwana Yesu Kristo aliyetufia msalabani. Karibu tuweze kujuzana yale yaliyojiri madhabauni mwa Bwana katika siku hii ya leo, ikiwa ni alhamisi ya kwanza kabisa ya mwaka 2014.
Leo kama kawaida ibada ilianza kwa sifa na kuabudu na baada ya muda, Mzee wa Upako alipanda madhabahuni na kuanza kuhudumu.
Baada ya kuongoza nyimbo za kuabudu na kusifu kama ilivyo kawaida yake, Mzee wa upako aliendeleza utabiri wake wa mwaka jana mwishoni, yaani wiki iliyopita, wa kuwa maisha ya kila mmoja atayaombea ili yaweze kubadilika, na kusema kuwa ataupika mwaka huu ili mambo yawe DOUBLE DOUBLE, kisha akausindikiza utabiri huo kwa mahubiri ya jinsi Mungu alivyo mtumia Musa katika kuwaokoa wana wa Israeli.
Aidha mtumishi wa Mungu, Mch. Antony Lusekelo, alitoa mfano wa Samson pia wa jinsi alivyorudiwa na nguvu zake baada ya nywele zake kuanza kuota tena, na kusema kuwa kama ilivyokuwa kwake Samson ndivyo Mungu atakavyorudisha upya nguvu zetu za kiuchumi, mipango, afya na kadhalika ndani ya mwaka huu wa 2014.
Na baada ya mahubiri hao yaliyochukua saa mbili, mtumishi wa Mungu aliwaongoza watu katika ibada ya matoleo, na kisha kuwaombea mmoja mmoja mpaka mwisho wa ibada.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa leo ibadani, japo kwa kifupi. Karibu sana Jumapili ili ujifuze mengi yatakayo kujenga kiakili, kiroho na hata kimwili.
Barikiwa sana!











